Here's the presentation that was given at the February network meeting by Alex Mayunga:
USHAWISHI NA UTETEZI KATIKA UKUSANYAJI WA RASILIMALI NA
RASILIWATU
Imeandaliwa na
Alex Mayunga
alexmayunga@gmail.com
Simu: 0713 547996
Tafsiri:
*
Ushawishi(Lobbying) na Utetezi (Advocacy) ni dhana zinazotumika pamoja na
wanaharakati wengi.
* Utetezi ni
kupigia debe ama kuunga mkono masuala ambayo unayaamini
* Ushawishi ni
mchakato unaobuniwa ili kuepika mawazo ya wafanya maamuzi ili kupata uungwaji
mkono wa programu ama mkakati .
* Maamuzi haya
huweza kuwa ya kisera, mkakati, sheria ama rasilimali.
* Ushawishi
unalenga kuleta mabadiliko ya kimaslahi ama matakwa ya wadau mbalimbali ili
yaendane na matakwa ya kikundi husika
kama
vile Asasi, Mtandao wa asasi n.k
UCHAMBUZI WA NGUVU,UDHAIFU, FURSA NA
VIKWAZO KATIKA AZISE/MITANDAO MBALIMBALI.
NGUVU
q Uzoefu wa
shughuli za asasi za kiraia
q Uwezo mkubwa
unaotokana ushiriki mkubwa wa warsha,
semina na makongamano mbalimbali.
q Timu ndogo
lakini zenye watendaji wa kujitolea.
q Mazingira ya
kijiografia.
q Kuwa na
mtandao mpana wa taarifa na shughuli,
q Kuwa karibu na
wadau mbalimbali
kama
idara, taasisi za
serikali, washirika wa maendeleo n.k
q Mtazamo chanya
wa wadau juu ya umuhimu wa uwepo wa AZISE na Mitandao
UCHAMBUZI WA NGUVU,UDHAIFU, FURSA NA
VIKWAZO KATIKA AZISE/MITANDAO MBALIMBALI.
UDHAIFU
q Ukosefu wa
Rasilimali
Mf. Fedha,
vitendea kazi, watendaji wenye ujuzi na uzoefu
q Mifumo ya
upatikanaji wa Viongozi. Mfano: Kupigiwa kura ama kuteuliwa bila kuzingatia
vigezo.
q Kutokuwa na
viwango vinavyotambulika vya viongozi wa AZISE
q Uchanga wa
baadhi ya AZISE
q Kutamani
kutumia kila fursa inayopatikana.
UCHAMBUZI WA NGUVU,UDHAIFU, FURSA NA
VIKWAZO KATIKA AZISE/MITANDAO MBALIMBALI.
FURSA
* Kuwa na mitandao
na mashirika mengi yanayofana kimalengo na dira.
* Uwepo wa wadau
mbalimbali
kama
viongozi, wafanyabiashara na
wadau wa maendeleo .
UCHAMBUZI WA NGUVU,UDHAIFU, FURSA NA
VIKWAZO KATIKA AZISE/MITANDAO MBALIMBALI.
VIKWAZO
* Kukosa uungwaji
mkono wa moja kwa moja na wadau muhimu.
* Mtazamo hasi wa
jamii juu ya AZISE.
* Hofu ya utendaji
mbovu wa baadhi ya asasi.
* Ushindani mkubwa
wa AZISE/MITANDAO inayofanana.
* Ukubwa na uwezo
wa kirasilimali na rasiliwatu.
* Hofu ya ukosefu
wa uadilifu kwa baadhi ya watendaji wa baadhi ya wadau wa maendeleo.
* Tofauti za
shabaha kati ya AZISE na Wadau wa Maendeleo.
KWA NINI STADI ZA USHAWISHI NI MUHIMU?
* Kuwa na stadi
muhimu za ushawishi kunatuwezesha kuweza kuwekeza zadi katika maeneo ambayo
tuna nguvu, kurekebisha udhaifu wa kiasasi, kutumia vizuri fursa zilizopo na
kusaka nyingine na kikubwa zaidi kuepukana na vikwazo.
* Kumbuka si kila
changamoto katika AZISE / Mitandao zinasababishwa na Ufinyu wa Rasilimali na Rasiliwatu.
MAMBO MUHIMU KATIKA KUKUSANYA RASILIMALI
Mingi ya miradi au shughuli ina gharama. Baadhi itahitaji
kiasi kikubwa cha rasilimali na mengine kiasi kidogo cha rasilimali au mikakati
kidogo ya kukusanya rasilimali.
Mambo ya Kuzingatia
* Makisio ya
gharama kwa ajili ya shughuli/mradi.
* Wadau ambao
wanaweza kuchangia wataalamu, vifaa au/na pesa.
* Mpango madhubuti
wa kukusanya rasilimali/rasiliwatu katika maeneo yenye upungufu.
* Mchango wa
Washiriki ama watu watakaonufaika na mradi/shughuli
DONDOO MUHIMU ZA USHAWISHI WA KUKUSANYA RASILIMALI /
RASILIWATU
* Kabla ya
kukutana na mdau wa maendeleo kwa ajili ya kuomba rasilimali ni muhimu
kujiuliza mawasli yafuatayo.
* Kwa nini
tunamfuata mdau A, B na C na sio D?
* Tunaweza kupata
mdau wa kuunga mkono wazo/mradi/shughuli yetu?
* Mdau anajua
lolote kuhusiana na asasi/mtandao wetu na shughuli zake?
* Tunajua
anajishughulisha na nini, maeneo ya kipaumbele, shabaha na malengo yake?
* Nani ataratibu
zoezi la ushawishi inapofikia hatua ya kuwasilisha maombi yetu?
* Mdau anategemea
nini toka kwetu?
* Kitu gani hasa
tunataka kuomba?
DONDOO MUHIMU ZA KUKUSANYA RASILIMALI
8. Hoja gani tunapaswa kujenga?
9. Tunajua shirika ama watu wa karibu wa mdau ambaye
wanaweza kumshawishi? Mf. Mbunge, Diwani, Meya n.k
10. Kiasi gani cha rasilimali/rasiliwatu tunapaswa kuomba?
Kiasi maalum ama makisio?
11. Kuna sababu ya kutokuomba kitu chochote cha ziada?
kama
vile mafunzo, vitendea kazi n.k.
12. Tunataka kuambata na kitu chochote kinachooneha
mafanikio yetu Mfano: Ripoti ya miradi iliyofanikiwa, Barua za pongezi toks kwa
wadau wengine, Majina ya walezi ama wajumbe wa Bodi ya Udhamini n.k
IPI NI NJIA BORA YA KUKUSANYA RASILIMALI:
MBINU YA USHIRIKELI au HOJA?
USHIRIKELI:
* Onesha katika
mawasilisho yako na jinsi unavyowasilisha kwamba unaamini unachokisema na
umejiridhisha kwamba ni muhimu. Kwa njia hii unaweza kumfanya Mdau wa Maendeleo
kuvutika na kujaribu kuvaa viatu vyako.
* Kuwa makini usije ukatumia hisia nyingi
ukaonekana unaomba hisani au kuonewa huruma. Unaweza kuonekana mwenye kuhitaji
sana
, usiye mkweli au
usiye na utaalamu.
HOJA
Mbinu hii inakupasa uwe mjengaji mzuri wa hoja zenye mashiko
kuonesha unajua umuhimu wa mradi wako. Usijikite kwenye kutoa ahadi ila onesha
jinsi gani unaweza kutekeleza mradi/shughuli yako
TUNAWEZAJE KUJENGA MAHUSIANO NA ASASI ZENYE FALSAFA TOFAUTI?
* Kujenga uhusiano
na mashirika ambayo tonatofautiana nayo katika falsafa ni jambo jema.
* Inaongeza sifa
kwa asasi, kuongeza uwezekano wa mafanikio katika baadhi ya maeneo mnayofanana
na kuvutia washirika wa maendeleo wapya.
* Hii huweza
kufanikiwa iwapo asasi yenu itafanya ushirika kwa kuvutiwa na masuala ya msingi na sio haiba za watu.
* Usiwashambuie
watu unatofautiana nao; Hoji wanayosimamia lakini usiwashambulie.
* Jadiliana nao
kirafiki na jikite zaidi kwenye masuala muhuimu.
* Kinyume chake
tatengeneza maadui ambao pengine ungeweza kushirikiana nao siku za usoni.
* Alika watu toka
asasi tofauti katika matukio yenu
Ahsanteni!