Our network constitution, translated into Kiswahili by Dr Joseph Mambo:
Download mtandao_wa_asasi_za_kiafrika_tanzania.doc
MTANDAO WA ASASI ZA KIAFRIKA TANZANIA.
AFCONET
KATIBA
JINA: KATIBA YA MTANDAO WA ASASI ZA KIAFRIKA TANZANIA.
1.0 KIFUNGU CHA KWANZA.
1.1 JINA NA ANWANI
Jina la chama litakuwa AFRICAN COMMUNITIES NETWORK OF TANZANIA.(AFCONET)
1.2 Makao makuu ya chama yatakuwa Dare s salaam.
1.3 Anwani ya posta:
S.L.P 16559,
Kariakoo,
Daressalaam.
2.0 KIFUNGU CHA PILI.
MUUNDO WA CHAMA.
2.1 AFCONET Ni mtandao wa vyama visivyo vya kiserikali, ambavyo ni vya kujitolea, visivyo vya kisiasa ,kidini,kikabila na visivyotengeneza faida.
3.0 KIFUNGU CHA TATU.
MALENGO NA MADHUMUNI.
Malengo na madhumuni ya chama hiki ni:
3.1 Kukuza mawasiliano na ushirikiano na asasi
nyingine.
3.2 Kuwajengea uwezo wana mtandao.
3.3 Kushirikiana na asasi nyingine katika kuleta maendeleo na ufanisi mzuri kwa kujenga mahusiano mazuri kati ya asasi na asasi hivyo kukuza jina la chama kwa ujumla.
3.4 Kutetea haki za binadamu na kuondoa unyanyapaa wa aina yoyote ile.
4.0 KIFUNGU CHA NNE.
UANACHAMA
Kutakuwepo na aina tatu za uanachama.
4.1 Wanachama waanzilishi.
4.2 Wanachama wa vikundi/ushirika.
4.3 Wanachama wa heshima.
4.1.1 Wanachama waanzilishi.
Wanachama waanzilishi ni wale wa kwanza thelathini ambao wametokana na asasi zilizoko mkoani Dar es salaam ambao wametimiza masharti ya Argentarius foundation African communities (uk)(uingereza) katika mpango wake na mgawanyo wa kuanzisha mitandao.( AFCONET)
4.2.1 Wanachama wa vikundi / ushirika.
Nafasi zitakuwa wazi kwa asasi nyingine ambazo zitapendelea kujiunga na mtandao wa AFCONET.
Na watajadiliwa na kupitishwa na kamati ya utendaji ikishirikiana na viongozi wa Argentarius foundation African communities programme.
4.3.1Wanachama wa heshima
Wanachama wa heshima watakuwa ni wale waliotunukiwa uanachama kutokana na mchango wao mkubwa katika kujenga mtandao.
KIFUNGU CHA TANO.
HAKI NA WAJIBU WA MWANACHAMA
0.Kufanya/kutekeleza malengo na madhumuni ya mtandao.
1. Kufuata kanuni na sera za chama na vipengele vyake.
2. Kuchagua na kuchaguliwa kushika nyadhifa mbalimbali za uongozi katika katika chama.
KIFUNGU CHA SITA.
KUKOMA UANACHAMA.
1.Uanachama utakoma pale wanachama wa mtandao watakapopiga kura ya kumkataa mwanachama.
Kura za kumkataa mwanachama lazima zitolewe kwa makubaliano ya pamoja na chama cha Argentarius Foundation wakishirikiana na kamati ya utendaji ya mtandao (afconet)
2.Kushindwa kutekeleza sera ya chama na ukosefu wa nidhamu, kama vile, kushindwa kwa mwanachama kuhudhuria vikao vitatu mfululizo bila ya taarifa na bila ya maelezo ya kuridhisha.
3.Matumizi mabaya ya fedha ni kigezo cha kufutwa uanachama.
KIFUNGU CHA SABA.
LUGHA
Lugha ya mawasiliano kiofisi itakuwa ni KIINGEREZA na KISWAHILI.
Jitihada zitafanyika kwa kila mwanamtandao kuona kwamba lugha ya Kiswahili imepewa kipaumbele.
Sambamba na hilo wanachama wanakaribishwa kuwasiliana kwa kiingereza.
KIFUNGU CHA NANE.
MHIMILI WA MTANDAO.
1Watendaji wakuu.
2 Kamati ya utendaji
3 Mkutano mkuu wa mwaka.
KAZI ZA WATENDAJI WAKUU/VIONGOZI WA MTANDAO.
8.1.1Kutakuwa na timu ya watendaji wakuu wa mtandao.Mgawanyo wa kazi utakuwa kama ifuatavyo:
i. Mwenyekiti
ii. Katibu/mratibu
iii.Mweka hazina
8.1.2 Kamati ya utendaji itaandaa agenda za mikutano ya kila mwezi na zile mkutano mkuu.
8.1.3 Kamati ya utendaji itachaguliwa kila mwaka.
KAZI ZA KAMATI YA UTENDAJI
8.2.1
(i) Ni chombo kikuu katika kutekeleza kazi za mtandao.
(ii) Viongozi saba waliochaguliwa na mkutano mkuu.
Kamati hii itafanya kazi zifuatazo:
1.Kupanga, kusimamia, na kufanya tathmini kufuatana na malengo ya mtandao.
2. Kutoa rasilimali kwa wana mtandao.
3.Watawajadili wanachama wapya wakishirikiana na makao makuu ya mtandao (Argentarius) na kuwapitisha.
4.Idadi ya watendaji wakuu kwenye vikao lazima iwe 2/3 ya wanachama.
KAZI ZA MKUTANO MKUU.
Kutakuwepo na mkutano mkuu mara moja kwa mwaka.
8.3.1 Uchaguzi wa viongozi wote utafanyika katika mkutano huo.
8.3.2 Taarifa kwa wanaopendelea kugombea sharti ziwakilishwe kwa kamati ya utendaji mwezi mmoja kabla ya uchaguzi mkuu.
8.3.3 Taarifa ya uchaguzi wa viongozi hao ikiwa ni pamoja na majina ya wagombea lazima zitolewe wiki mbili kabla ya uchaguzi mkuu.
KIFUNGU CHA TISA.
UTARATIBU WA FEDHA ZA MTANDAO
Wanachama wa mtandao itawabidi wazingatie taratibu za fedha za mtandao.
9.1 Vitabu vyote vya mahesabu vitahifadhiwa kwenye ofisi ya mtandao.
9.2 Matumizi ya fedha na mtiririko wake utachapishwa na kusambazwa kwa wanachama wa mtandao.
9.3 Watia sahihi kwenye vitabu vya mahesabu na benki watatokana na kamati ya utendaji.
Hakuna mwanachama katika kamati ya utendaji kwa jina la mtandao atakayejinufaisha mwenyewe au wale anaohusiana nao moja kwa moja kama vile ndugu,mzazi,mtoto,mke au mume, marafiki n.k bila ya kutoa taarifa juu ya kitendo hicho kwa mwezeshaji wa msingi yaani ARGENTARIUS na kwa wanachama.
9.4 Mtandao utafanya shughuli zake katika misingi ya kutozalisha faida, au kushirikiana na mamlaka ya mapato Tanzania kimkataba.
KIFUNGU CHA KUMI.
KURA
10.1Kila mwanachama wa mtandao anao wajibu wa kupiga kura moja kwenye mkutano.
10.2 Iwapo kuna wawakilishi wawili toka kwenye asasi moja, basi asasi hiyo itamchagua mmojawao awe ndiye mwakilishi wao katika mkutano huo.
10.3 Kura zote zitakuwa ni za siri.
KIFUNGU CHA KUMI NA MOJA.
MAREKEBISHO YA KATIBA.
11.1 Marekebisho ya katiba yanaweza kufanyika kwa idadi ya theluthi mbili za wanachama (2/3) wakati wowote iwapo ni lazima.
11.2 Taarifa kuhusiana na marekebisho ya katiba inabidi taarifa hizo ziwafikie wanachama angalau siku 14 kabla ya mkutano mkuu.
KIFUNGU CHA KUMI NA MBILI.
KUVUNJA CHAMA
12.1 Mtandao unaweza kuvunjwa au kufutwa kufuatia maazimio yaliyofikiwa kwa idadi ya asilimia 2/3 ya wanachama wote kwenye kikao au mkutano mkuu usio wa kawaida ulioitishwa kwa ajili hiyo tu.
12.2 Pale ambapo makubaliano yamepitishwa ya kuvunja mtandao, mkutano mkuu huo ambao sio wa kawaida (EOG Meeting) utamteua mtu au bodi ya watu watakaokuwa wafilisi na watafanya hivyo kama hatua ya mwisho ya kukabithi rasilimali za chama na itafanya maamuzi kuhusu mali za mtandao chini ya kamati ya utendaji kwa makubaliano na ARGENTARIUS ambao ndiyo watakaotoa uamuzi wa mwisho kuhusiana na maamuzi hayo.
Orodha ya wanachama waanzilishi wa mtandao huu ambao wameridhika na katiba hii:
namba
Jina la asasi
Majina ya viongozi
Anwani/simu
Sahihi
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30

Comments