Maelekezo ya kutembeleana kwa kubadilishana uzoefu
Download fomu_ya_maelezo_ya_kutembeleana_ya_kiswahili.doc
(Also available in English.
Mtandao wa taasisi za kijamii Dar Es Salaam
Mpango wa Ruzuku wa mwaka 2007
Kablasha hii inaelezea kwanini ni muhimu, nakinachofanya kutembeleleana kwa kubadilishana uzoefu kufanikiwa na jinsi ya kutembeleana na kudai gharama zilizotumika
Kwanini kutembeleana kwa kubadilishana uzoefu kunajalisha
Katika Dar Es Salaam kuna dazani au bila shaka hata mamia ya vikundi vinavyo wasaidia yatima na Watoto wanaoishi katika mazingira magumu walioathirika na UKIMWI.
Lakini kuna uratibu mdogo kati yao na matokeo yake kikundi kimoja kinapojifunza mambo mara zote hawafundishi vikundi vingine
Nia ya Mtandao wetu in kuimarisha vikundi vyenu na njia muhimu ya kufanya hivi ni kuwasaidia kujifunza kutoka kwa kila kikundi
Ni vema kukutana kila mwezi katika mkutano, lakini njia bora ya kujifunza ni kuwatembelea wengine na kuona kwa macho yako mwenyee wanavyofanya.
Malipo kwa matembezi ya kubadilishana uzoefu
Tuna thamini kuwa unapofanya matembezi ya kubadilishana uzoefu wajumbe wa kikundi chako wanajitolea muda wao.Kwa hiyp mwaka 2007, tutawalipa gharama ambazo kwa hakika zimetumika (basi au dala-dala) kwa idadin ya waliotfanya matembezi kenda na kurudi) na nyongeza ya TZS 4000 kama watu wawili au zaidi watakuwa wamfanya matembezi ya kujifunza. Kwa mfano kama wataenda watu watatu watapata TZS 4000 pamoja na nauli yao wote watatu. Kama kaenda mmoja tu atapata TZS 7000 pamoja na nauli aliyotumia una ruhusiwa kutumia peas hii katika chakula au kitu kingine chochote.
Kinachofanya mafanikio ya kutembeleana
Tulijifunza kutoka mwaka 2006 baadhi ya mambo yaliyofanya mafanikio
? Idadi ya kutosha ya watu toka pande zote walihusika katika mazungumzo
? Muda wa kutosha kujadili kazi unazofanya na kuona kwa macho yako za wengine.
? Juhudi za kuashirikisha wanakikundi wenzako unaporudi kikundini
? Mazingra ya kufaa/rafiki katika mkutano
? Juhudi za kutaka kujifunza badala ya kupiga soga
? Kutembeleana kumekuwa shirikishi kwani si watu walewale kutoka kikundini
Jinsi ya kupanga kutembeleana
Njia rahisi ni kupang ana kikundi wakati wa mikutano ya kila mwezi ya wana mtandao.Ongea na wanakikundi unachotaka kukitembelea mkubaliane tarehe na muda. Kama utashindwa kufanya hivyo wapigie simu na uwaombe wapendekeze tarehe na muda kati ya siku mili au tatu ambazo ni sahihi kwao kutembeleana. Kikundi unachotembelea angalau kiwe na watu wawili au watatu ambao utaongea nao kuwa tayari kukuonesha taarifa na kama inawezekana unawezan kwenda wakati unapoweza kushuhudia shughuli zao wakati zikifanyika. Mkishakubaliana na kikundi baada ya kukupa uchaguzi wa siku na muda ongea na wanakikundi wenzako na kuwajulisha siku mliochagua kati ya zilizopendekezwa.
Thibitisha kutembeleana kwa wenyeji na muwasiliane kama umechelewa
? Watembeleaji watume ujumbe wa maneno mafupi ya simu siku moja kabla ya kufika na wenyeji wajibu kuthibitisha kuwa ni SAWA.
? Inaonesha kujali na uungwana kufika kwa wakati baadala ya kuwa weka wengine muda mrefu wakikusubiri.Kama unachelewa watumie ujumbe wama maneno mafupi ya simu au wapigie simu ukiwajulisha kuwa utachelewa.Usingoje mpaka wakati ambao kiakao kinastahili kuanza.
Namna ya Kunufaika matembezi ya kubadilishana uzoefu.
? Usisahau kuchukua fomu ya taarifa ya kutembeleana
? Chukua kalamu na karatasi
? Kwa mara ya kwanza kila mmoja atajitambulisha. Hii ni muhimu kwani mnaweza kuwa mmeonana katika mkutano wa kila mwezi wa Mtandao, pengine mmesahau majinahis.. Eleza kazi yako –Mfano Mwenyekiti, Mhazini,Mratibu, Mtu wakujitolea au Katibu.
? Andika majina na namba za simu katika fomu ya taarifa.Hii itasaidia mkitaka kuwasiliana..
? Inapendeza kama wenyeji watawapa viburudisho
? Jaribu kujifunza kinachofanywa na kikundi kingine. Angalia kama kikundi chenu mnaweza kujifunza kutoka kwao.
? Jaribu kukieleza kikundi hicho mawazo bora unayodhani yanwezan kuwafaa.
? Andika dondoo wakati wa majadilianao katika fomu ya tarifa ya kutembeleana
? Kabla ya kuondoka, waombe wenyeji wasini fomu ya taarifa ya kutembeleana
? Unapokuwa umerudi katika kikundi chaon fanya kikao kuwaeleza ulichojifunza. Mjadili ni mabadiliko yapi mnaweza kufanya katika kikundi.
Kupata Malipo Kutokana na kutembeleana
? Tembelea kikundi kipa, si ulichokwisha tembelea kwa mwaka 2006. Kama unataka kutembelea kikundi kilicho kutembelea, tafadhali tuma barua pepe kwa Tim kabla ya kukitembelea (tim at africancommunities dot org) uelezee kwanini unadhani utajifunza zaidi kwao kuliko kikundi ambacho hamjaonana.
? Asiwe mtu yule yule anaye tembelea vikundi kutoka katika kikundi kimoja. Ni bora kuwashirikisha kwa kubadilishana miongoni mwa watu wote muhimu katika kikundi kutembelea vikundi. Kwa jinsi hii wanakikundi wote watakuwa wamejifunza
? Tafadhali tumia anagalau muda wa saa mbili katika kikundi ulichotembelea
? Jaza fomu ya taarifa ya kutembeleana wakati mkutano, na itiwe sahihi na wenyeji na kasha uilete siku ya mkutano wa mwezi wa mtandao

Comments