Wapendwa Wanamtandao,
Ninatazamia sana
kuonana nanyi ndani ya kipindi cha wiki
moja ijayo wakati natembelea Dar es Salaam. Hapa kuna taarifa iliyofupishwa ya
shughuli za mtandao kwa sababu natarajia kupata wasaa wa kuongea na kila mmoja
wenu ana kwa ana.
Pikiniki ya Watoto
Tunaelewa kwamba bado mnaendelea
kujadiliana kuhusu jambo hili na mipango bado inaendelea, lakini hatujui kama
tayari mmeshapanga tarehe au mipango yenu ni ipi.
Sisi huku London
tunaunga mkono wazo hili sana
na tunatumaini
kwamaba mnaendelea kutafuta suluhu nzuri kwa tatizo la kuwakatisha tamaa watoto
ambao hawatapata nafasi ya kushiriki kwa sababu ya idadi kuwa finyu.
Akaunti ya Benki na rekodi za fedha
Tunaelewa kwamba akaunti ya benki
tayari imeshahamishwa, lakini hatujapata taarifa yeyote kutoka kwa mtunza
hazina juu ya jambo hilo
.
Pia tunasubiria jibu kutoka kwa mtunza hazina kwa baadhi ya maswali kuhusu
akaunti. Maswali haya ni muhimu sana
kwa sababu
tunapaswa kuwaonyesha wadhamini wetu huku London
jinsi fedha zilivyotumiwa na mtandao kabla hatujafanya malipo ya ruzuku ya 2008
kwa vikundi vyenu, hivyo tafadhali fanyeni kila muwezalo kumsaidia mtunza
hazina kujibu maswali yetu.
Ziara za kwenye vikundi
Taarifa ya hivi karibuni kutoka kwa
Donatian, ya kabla ya mwisho wa wiki iliyopita ambayo haihusishi ziara za
tarehe 17 na 18 Novemba, ni kwamba, vikundi 15 tayari vimeshatembelewa, lakini
mpaka sasa Donatian hajapata taarifa kamili kutoka kwa kikundi chochote kile.
Tuko makini sana
katika kuhakikisha kwamba vikundi vyenu vinapata hundi ya ruzuku kwenye mkutano
wa mwishoni mwa mwezi Desemba, lakini hili linawategemea ninyi mtoe taarifa
muhimu zinazohitajika ili ruzuku iidhinishwe. Kwa jinsi inavyoonekana mpaka
sasa ni kwamba wengi wenu hamtastahili kupata ruzuku, labda mpaka mwanzoni mwa
mwaka ujao. Tafadhali naomba mharakishe kutoa taarifa zote ambazo Donatian
amewaagiza.
Mkutano wa Mtandao wa Mwezi Novemba
Furaha anaandaa kipindi kwa ajili
ya mkutano wa Novemba ambapo anategemea kwamba mtapatiwa uwezo wa kujaza
taarifa fupi kwa Kiswahili ya shughuli za kikundi chenu kwa 2007. Hii itakuwa
ya manufaa sana
hasa kwa vikundi ambavyo bado havina taarifa ya mwaka na taarifa hiyo pia itawasaidia kujaza ukurasa mmoja wa ile
fomu yetu ya Ruzuku.
Mkutano wa Mtandao kwa tarehe 2 Desemba
Tumepanga tuwe na mkutano maalumu
siku ya Jumapili tarehe 2 Desemba. Hii itahusisha uchaguzi wa viongozi wapya wa
mtandao ili kuhudumia mtandao kwa 2008, na pia majadiliano ya wazi kuhusu
mstakabali wa mtandao wetu, ambapo natumaini mtaamua ni shughuli gani mngependa
mtandao ufanye kwa mwaka ujao na mwaka utakaofuata ambao utakuwa mwaka wa
mwisho wa programu yetu ya ruzuku. Tumegundua kwamba kwa wengi wenu, jumapili
ni siku ambayo kwa kawaida mnatumia muda wenu kushinda na familia, na kwa namna
ya pekee tunashukuru kuona kwamba mmedhamiria kuja kwenye mkutano kwa siku
hiyo. Asanteni sana
.
Mradi wa Maktaba;
Steven Milambo amefanya
mabadiliko kwenye azimio la kuomba ruzuku baada ya majadiliano kati yenu kwenye
mkutano wa mtandao na sisi huku London
.
Tunatarajia kushughulika naye pamoja na YLRF kuhakikisha kwamba hilo
azimio linafika kwa
mashirika lengwa ambayo yanaweza kufadhili. Kama
mnavyojua kati ya changamoto juu ya kuwa na maktaba moja kubwa ni kwamba watoto wakaao mbali na maktaba
hiyo watapata ugumu wa kufika. Kama
tutafanikiwa kupata ruzuku kwa ajili ya mradi huu,
hapo mapango utakuwa ni kila kikundi ndani ya mtandao kipewe na mkusanyiko
mdogo wa vitabu vya kiaada. Vitabu hivi vinaweza kutunzwa kwenye ofisi za
vikundi vyenu ili watoto waweze kufika na kuvitumia.
Tafadhali jibu ombi langu la kutembelea vikundi kwa Desemba 3 na
kuendelea
Ili
kuweza kutembelea vikundi ambavyo sikuvitembelea mwaka uliopita, nimetuma
ujumbe kwa vikundi nikiwaomba uwezekano
wa kuwatembelea katika ofisi zenu mwaka ujao. Baadhi ya vikundi tayari
vimeshatoa jibu la ndiyo: Chakupau, YLRF, Vumwe, pofideso.
Hapa kuna orodha ya wale ambao
hawajajibu; nitafurahi sana
kama
mtaweza kumwambia Donatian au Furaha kwenye mkutano ili waweze kunijulisha
kwamba mko tayari kutembelewa nami na kwamba viongozi wa vikundi vyenu
watakuwepo.
|
Jina la mtu au la kikundi
|
Date/tarehe
|
Time/muda
|
|
Sageta
|
Jumatatu 3 Desemba
|
3 asubuhi
|
|
Poverty Fighters
|
Jumatatu 3 Desemba
|
7:30 Mchana
|
|
Donatian Marusu
|
Jumatatu 3 Desemba
|
10 jioni
|
|
Preventive Healthcare Frontiers
|
Jumanne 4 Desemba
|
3 asubuhi
|
|
Twafaha
|
Jumatano 5 Desemba
|
3 asubuhi
|
|
Moms in Touch
|
Jumatano 5 Desemba
|
5:30 asubuhi
|
|
Chiyowonet (pamoja na Yopac na Tupendane Kujadili kuhusu mradi
shirikishi)
|
Jumatano 5 Desemba
|
8 mchana
|
|
Yovita Makoko
|
Alhamisi 6 Desemba
|
1:30 asubuhi (Kivukoni)
|
|
Chimaba Sanaa (pamoja na Nice na Wolisu, kujadili kuhusu mradi
shirikishi) – sina uhakika kama huu mkutano
umekubalika
|
Alhamisi 6 Desemba
|
3 asubuhi
|
Je, ungependa kuambatana nami katika ziara za kwenye vikundi?
Kama wewe (au mwanachama mwingine
wa kikundi chenu) angependa kusafiri nami katika kutembelea vikundi kipindi cha
ujio wangu, basi mpe jina lako Donatian (au Furaha kama
hayupo) na onyesha ni siku gani ungependa. Mtapaswa kuja Kivukoni saa 2:45
asubuhi kuanza safari, chakula cha mchana kitakuwepo, na mtapokea malipo kidogo
kwa muda mtakaoutumia. Ziara zitakoma sa 10 jioni.
Je, mngependa kutembelewa?
Kama mngependa kutembelewa nami,
basi mwambie Donatian (au Furaha, kama hayupo) na nitaona kama
nitafanikiwa kupanga ziara hizo.
Shughuli za viongozi;
Hatujapokea bado taarifa yeyote
ile kutoka kwa viongozi inayoonyesha kwa mhutasari shughuli zao kwa mwezi huu.
Kutembeleana katika vikundi
Jumla ya ziara zote zilizofanywa
mwaka huu ni 163. Vikundi ambavyo havijakamilisha ziara sita (kwa mjibu wa
taarifa tulizopokea mwishoni mwa mwezi Octoba) ni:
- Chiyowonet
- Good Samaritan Foundation
- Iyana Education Trust
- National Youth Information Centre NICE
- Preventive Healthcare Frontiers*
- Red House 2000
- Sageta Youth and Children
- Sinza Youth Peer Educator*
- Tai Women Support Group (Tawosu)
- Tukolene Youth Development Centre
- Tupendane women group
- Twafaha Women Action Fighters v AIDS*
- Upendo Group
- WOLISU Women Life Support Network
- WOYONA Women Youth Nature Action
Vikundi vilivyowekewa nyota
kwenye majina yao
(*) vimefanya ziara chache sana
chini ya nne
zilizoripotiwa. Kupokea ruzuku ya 2008, vikundi vyenu vitapaswa kuwa tayari
vimefanya jumla ya ziara sita (6) kwa mwishoni mwa 2007 (na kuwasilisha kwa mtindo
wa taarifa!) tafadhali mfanye bidii.
Nawatakieni nyote mafanikio mema,
Tim
Na kutafsiriwa na
Donatian Marusu
23/11/2007