MPANGO MKAKATI
* Taasisi moja yaweza kutumia rasilimali nyingi ili ziweze kushindana na taasisi zingine. Rasilimali hizo ni kama vile:
* Mitambo, vifaa, teknolojia
* Muundo wa taasisi husika, mahusiano kazini, mifumo ya upangaji, tathmini na ufuatiliaji
* Rasilimali watu (ujuzi, uzoefu na tabia)
* Kwa kawaida rasilimali ambazo taasisi inamiliki ndizo huweza kuipa uwezo wa kushindana na taasisi zingine katika mazingira ambamo taasisi husika imo.
* Kwa hiyo lengo kuu la mpango mkakati ni kusaidia kugawa rasilimali kwa uangalifu ili ziweze kusaidia kushindana na taasisi zingine katika mazingira.
MAANA YA MPANGO MKAKATI
* Mpango Mkakati ni mpango wa jumla wa maendeleo ya taasisi husika unaopangwa kwa kuzingatia mambo yafuatayo:
* Changamoto zinzoikabili taasisi husika katika mazingira ya ushindani
* Hali halisi ya mazingira ambamo taasisi hiyo imo
* Uwezo wa taasisi husika katika kutekeleza majukumu yake
* Dira, dhamira na malengo ambayo taasisi imejiwekea
* Sera na sheria za nchi zinzotawala shughuli za taasisi husika
* Mpango mkakati unahusisha mchakato wa kuchanganua hali ya ushindani wa taasisi, kutayarisha dira, dhamira na malengo ya taasisi, kuandaa mpango wa utekelezaji na kutafuta rasilimali zitakazosaidia kufikia malengo yaliyowekwa.
MCHAKATO WA KUTAYARISHA MPANGO MKAKATI
* Mchakato wa kutayarisha mpango mkakati kwa kawaida hufuata hatua kuu nne muhimu kama ifuatavyo:
(a) Uchanbuzi wa hali halisi
* Ni ipi hali halisi ya taasisi kwa sasa?
* Hatua hii inahusisha uchambuzi wa taasisi yenyewe na mazingira yanayoizunguka
* Lengo la kuichambua taasisi husika ni kufahamu uwezo (strengths) na udhifu (weaknesses) wake. Uchambuzi huu hufanywa kwa kuangalia dira, dhamira na malengo ya taasisi husika.
* Lengo la kutathmini mazingira yanayoizunguka taasisi ni kutaka kupata ufahamu wa fursa (opportunities) na vikwazo (threats) vya taasisi husika.
Swali: Chambua hali halisi ya taasisi yenu
(b) Uandaaji wa mpango mkakati
* Taasisi inataka kuwa ya namna gani?
* Kutayarisha dira, dhamira na malengo ya taasisi
* Kuandaa mpango wa maendeleo ambao unaonyesha malengo, matendo, muda wa utekelezaji, wahusika, rasilimali na viashiria vya ufanisi
Swali: Fafanua dira na dhamira ya taasisi yenu
Swali: Ainisha viashiria vya ufanisi katika utendaji wa taasisi yenu
Mfano wa mpango wa muda mrefu (long term development plan)
Lengo
Shughuli
Matendo
Muda
Mhusika
Rasilimali
Maoni
A
B
C
D
Kuboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia
Kujenga vyumba 3 vya madarasa ifikapo mwaka C
-Kuhamasisha jamii
-Kutenga eneo la ujenzi
-Kubaini mahitaji na gharama
-Kutafuta fedha
-Kuandaa ramani
-kujenga vyumba 3 vya madarasa
-K/shule
-Jamii
-Wahisani
-H/ Wilaya
-Serikali kuu
-Fedha
-Nguvu kazi
-Vifaa
Kujenga maabara 2 ifiakapo mwaka D
-Kuhamasisha jamii
-Kubaini mahitaji na gharam
-Kutafuta fedha
-Kuandaa ramani
-kujenga maabara 3
-K/shule
-Jamii
-Wahisani
-Serikali kuu
-Fedha
-Nguvu kazi
-Vifaa
(c) Utekelezaji wa mpango
* Taasisi itafikaje kule inakotaka kufika?
* Wakati wa utekelezaji wa mpango sharti taasisi izingatie muundo wake wa utendaji, kugawa rasilimali kwa kufuata vipaumbele, kuhakikisha kuwa watumishi waliopo wanatosha na wana ujuzi unaotakiwa.
* Mpango wa utekelezaji wa mwaka pamoja na bajeti huandaliza kwa kuzingatia uwezo wa taasisi husika
* Baada ya fedha za utekelezaji kupatikana mpango kazi huandaliwa ukiwa ni mwongozo wa utekelezaji
Swali: Chora muundo wa taasisi yenu
Mfano wa mpango wa muda mfupi (short term development plan)
Shughuli
Matendo
Muda wa Utekelezaji
Mhusika
Rasilimali
Maoni
J
F
M
---
D
Kujenga chumba 1 cha darasa
-Kuhamasisha jamii
-Kamati ya shule
-Serikali ya kijiji
-Fedha
-Nguvu kazi
-Kutenga eneo
-Kamati ya shule
-Nguvu kazi
-Kubaini mahitaji na gharama
-Kamati ya shule
-Nguvu kazi
-Vifaa
-Kutafuta fedha
-Kamati ya shule
-aserikali ya kijiji
-Fedha
-Nguvu kazi
-Vifaa
-Kuandaa ramani
-Kamati ya shule
-Serikali ya kijiji
-Fedha
-Nguvu kazi
-Vifaa
-Kujenga chumba 1 cha darasa
-Kamati ya shule
-serikali ya kijiji
-Fedha
-Nguvu kazi
-Vifaa
Mfano wa mpango kazi (action plan)
Shughuli
Matendo
Mhusika
Rasilimali
Maoni
J
F
M
A
M
J
--
D
Kujenga chumba 1 cha darasa
-Kusafisha kiwanja
-Mwalimu mkuu
Fedha na nguvu kazi
-Kununua vifaa
-Kamati ya shule
Fedha na nguvu kazi
-Kupima kiwanja
-Kamati ya shule
Nguvu kazi na vifaa
-Kuchimba msingi
-Kamati ya shule
Nguvu kazi na vifaa
-Kujenga msingi
-Kamati ya shule
-Serikali ya kijiji
Fedha, nguvu kazi na vifaa
-Kupandisha kuta
-Kamati ya shule
-Serikali ya kijiji
Fedha, nguvu kazi na vifaa
-Kuweka linta
-Kamati ya shule
-serikali ya kijiji
Fedha, nguvu kazi na vifaa
-Kujenga gebo
-Kamati ya shule
-serikali ya kijiji
Fedha, nguvu kazi na vifaa
-Kupaua
-Kamati ya shule
-serikali ya kijiji
Fedha, nguvu kazi na vifaa
-Kumalizia (finishing)
-Kamati ya shule
-serikali ya kijiji
Fedha, nguvu kazi na vifaa
(d) Ufuatiliaji na tathmini ya mpango
* Taasisi itajuaje kwamba imefika mahali ilipokusudia?
* Ufuatiliaji hufanywa ili kufahamu ni kwa kiasi gani taasisi imefikia malengo yake kwa kuzingatia dira na dhamira.
* Kwa kufanya ufuatiliaji na tathmini taasisi huweza kuchukua hatua za marekebisho pale ambapo mambo hayajaenda vizuri.
Swali: Ni zana ipi inatumika katika ufuatiliaji na tathmini katika taasisi yenu
Imetayarishwa na:
Salvatory R. Libery
Mob: 0787 693548
E-mail: libericha@yahoo.com
Halmashuri ya Wilaya ya Mvomero
S.L.P 690, MOROGORO

Comments