Taratibu za ruzuku ya 2008
Mtandao wa Jumuiya za Afrika za Dar es Salaam
(English version below)
Wanamtandao wapendwa,
Sisi shirika la Argentarius la London tunayo furaha kwamba mnafanya kazi kwa bidii za kuwasaidia watoto walio katika mazingira magumu ndani ya jamii.
Kwa mwaka uliopita, imekuwa bayana kwamba ni muhimu vikundi vyote ndani ya mtandao kufanya kazi kwa uwazi na uadilifu mkubwa. Njia bora ya kufanya hivyo ni kwa wanachama wa kila kikundi kuelewa vizuri vyanzo na matumizi ya fedha za kikundi.
Na ndiyo maana kwa kushirikiana na viongozi na kamati tendaji, tumetengeneza Mkataba wa Jumuiya za Afrika. Hayo ni makubaliano ambayo kila kikundi kitakachopata ruzuku kutoka shirika letu kitafanya ili kuongoza mwelekeo na tabia ya kikundi.
Ili kuufanya mkataba ufanye kazi na siyo maneno tu, tumeamua kuuweka kama masharti ya kupokea ruzuku mwaka huu kwamba mahitaji yafuatayo sharti yatimizwe:
Masharti ya kupata Ruzuku
* Mtafanya mkutano wa dakika 30 ambapo mtakabidhiwa hundi yenu
* Kuhakikisha kwamba watu wasiopungua 10 wamehudhuria
* Kuhakikisha kwamba viongozi wenu wote na wanakamati wanakuwepo(na
kama mmojawao hatakuwepo, basi mmweleze kaimu mratibu ili apate
kutuomba sisi huku London kutoa ruhusa maalumu ya kuwapa hundi ya
ruzuku)
* Watoto na familia jirani wakaribishwe kwenye mkutano huo
* Kabla ya mkutano muandae bango kubwa litakalokuwa na ujumbe wa mkataba wa jumuiya za Afrika na libandikwe kwenye ukuta
Kitatokea nini kwenye mkutano
* Naibu mratibu atakuja ofisini kwenu wakati mtakapokuwa tayari
* Naibu mratibu atampa kila atakayekuwepo karatasi itakayokuwa na anuwani
* Mtamwonyesha maelezo ya Mkataba
* Naibu mratibu atatoa hotuba fupi kuwapongeza kwa kazi zenu na kuelezea mkataba kwa yeyote atakayekuwepo
* Kutakuwa na dakika 5 kwa yeyote yule kuuliza maswali. Kama naibu
mratibu hatakuwa na jibu, basi swali hilo litatumwa kwa viongozi au
kwa shirika letu huku London
* Mtakabidhiwa hundi ya ruzuku na picha itapigwa
* Kila atakayekuwepo kwenye mkutano ataweka saini kwenye ahadi ya mkataba
* Hatimaye mkutano utafungwa rasimi, lakini yeyote atakayejisikia atakaribishwa kuendelea na maongezi baada ya hapo.
Grant Procedures for 2008
AfricanCommunities Network Dar es Salaam
Dear network members,
We at the Argentarius Foundation in London are happy that you are working so hard to help the most vulnerable children in society.
Over the past year, it has become clear that it is important for all groups in the network to act transparency and honestly. The best way to make sure of this is for the members of each group to understand clearly where the group’s money is coming from and going to.
That is why, working with the officers and executive committee, we have come up with the AfricanCommunities charter. This is a set of promises made by each group who receives funding from our foundation about how the group will behave.
To make the charter a reality rather than just a theory, we are making it a condition of receiving your grant this year that you meet the following requirements:
Requirements to get your grant
* You hold a 30-minute public meeting at which your grant cheque will be handed over.
* A minimum of 10 people are present at this meeting.
* All your officers and committee members are present. (If one cannot attend, please tell the deputy coordinator to ask us in London for special permission to give your grant cheque anyway.)
* Children and local families should be welcome to attend the meeting.
* Before the meeting, you prepare a big poster that contains the text of the AfricanCommunities charter and you stick it on the wall.
What will happen at the meeting
* The deputy coordinator will come to your office when you are all ready.
* The deputy coordinator will give everyone present a piece of paper with contact details on it.
* You will show the charter notice to the deputy coordinator.
* The deputy coordinator will make a short speech to congratulate you on your work and explain the charter to everyone who is present.
* There will be five minutes for anyone to ask questions. If the deputy coordinator does not know the answer, the question will be referred to officers or to the Foundation in London.
* The grant cheque will be handed over and a photo will be taken.
* Everyone present will sign the Charter Pledge.
* The meeting is then formally over, but anyone is welcome to stay and talk afterwards.

Comments