AFRICAN COMMUNITIES TANZANIA NETWORK
MKUTANO WA JANUARI 26, 2008
UKUMBI- CARE INTERNATIONAL
UFUNGUZI WA KIKAO:
Kikao kilifunguliwa na Mwenyekiti saa 3:40 asubuhi.
TAARIFA YA KIKAO KILICHOPITA:
Taarifa ya kikao kilichopita ilisomwa na Katibu Steven Milambo.
YATOKANAYO:
KUHUSU KATIBA:
Katiba imeandaliwa na Kamati Kuu tayari kwa kujadiliwa. Imependekezwa Katiba iwe katika lugha ya Kiswahili. Mkutano ulimwachia Katibu kuratibu suala la Katiba.
UTARATIBU WA BENKI:
Akaunti ya Benki ipo tayari na Mwenyekiti aliwasiliana na viongozi waliopita kukamilisha sualal la mahesabu ya fedha na benki.
MPANGO MKAKATI:
Tutafanya mapitio ya Mpango wa Mwaka ili kuweza kukidhi8 mahitaji ya wanachama. Mashirika machache yameleta mipango mikakati. Ni vigumu watu kufanya kazi kama hawana mpango wa kazi. Viongozi wamesisitiza kwamba yeyote mwenye tatizo juu ya kuandaa mpango kazi awasiliane na Katibu ili kuandaa mchakato wa kuwasaidia mapema iwezekanavyo.
MADA:
Umuhimu Wa Katiba katika maendeleo ya Asasi iliwasiishwa na Utti Mwang’anda kutoka CWCA.
- Alieleza juu ya uwajibikaji.
- Taratibu za masuala ya Utawala na Fedha.
- Muundo na mfumo wa Taarifa.
YALIYOJILI:
> Muda wa Uongozi.
> Wajibu wa Viongozi.
> Sera ya Fedha na Uongozi.
> Jina African Communities imesajiliwa Uingereza?
Kama imeasajiliwa – itabidi tufahamui taratibu za huko London.
> Mtandao hauna Dira na Muono.
> Tetengeneze Dira na Muono. (Haya yanaendana na Mkakati).
KUHUSU KUPUNGUA KWA FEDHA:
Yovita alitoa ufafanuzi juu ya tofauti kati ya taarifa ya Fedha na Taarifa za Benki. Yovita alizidisha 443,000 kimakosa. Alimtumia Timu kuhusu tofauri ya taarifa hizo. Mkutano umekubaliana.
KUHUSU CHIYOWONET:
Chiyowonet walikuwa hawajatuma CCAT Form.
Mkutano uliamua kwamba Argentarian Foundation watume taarifa kwa Viongozi mapema (Wiki moja kabla) kuwapa viongozi muda wa kupitia. Aidha mkutano umeomba Argentarian Foundation watoe maelezo ya kutosha.
KUHUSU TAFAHA NA YOVITA:
Yovirta alisema kwamba Tafaha walimfuata Ofisini kuomba wamwandikie ripoti ya Foundation For Civil Society.
Mradi wa Twafaha ulikua na kipengele cha malipo kwa ajili ya Mtaalam wa Mahesabu.
Mkutano uliamua uongozi wa AFCONET waandike barua kwa TWAFAHA kuomba taarifa na maelezo rasmi juu ya suala la malipo kwa YOVITA.
Kutembeleana kwa vikundi.
Hakukuwa na taarifa ya kutembeleana kwa vikundi.
Azimio la uwazi
Kikao kilipitisha azimio la uwazi kwa kura 24 za ndio na kura 0 za hapana.
Mengineyo.
Hakukuwa na mengineyo
Kufunga kikao
Kikao kilifungwa na mwenyekiti saa 11:30 jioni.
Imetayarishwa Kuhakikiwa na
Steven Milambo Jacka Mwambi
Katibu Mwenyekiti
