TAARIFA YA MKUTANO WA AFCONET
TAREHE 01/03/2008
UKUMBI WA CARE INTERNATIONAL
Ufunguzi wa kikao
Kikao kilifungulia na mwenyekiti saa saa 4:00asubuhi
TAARIFA YA KIKAO KILICHOPITA
Taarifa ilisomwa na katibu.
Kutembeleana kwa vikundi
Poverty Fighters walitembelea kikundi cha FAM kilipo nje ya mtandao. Donatian alifafanua juu ya utaratibu ju ya kutembeleana kwa vikundi. Mkutano uliamua kwamba watu wa Poverty Fighters wasilipwe pesa hiyo.
BARUA KUTOKA KWA
ARGENTARIAN FOUNDATION
Taarifa kutoka argentarian Foundation ilisomwa na Donatian.
Yaliyojili
Wanachama walihoji juu ya ya vitendo vibaya alivyofanyiwaVioleth. Walimwomba Violeth atoe ufafanuzi juu ya vitendo hivyo vibaya.
Viongozi walitoa ufafanuzi kwamba suala la Violeth limemalizwa katika vikao vilivyofanywa kati ya viongozi na Violeth.
Violeth alihakikishia mkutano kwamba
· Hakumshawishi Tim kutoa neti kwa Moms in Touch
· Hakutoa tafsiri ya uongo kwaTim
· Hakutuma taarifa za uongo kwenda foundation ya Argentarian Foundation
· About PHCF. Alisema kwamba hakuchangia lolote katika kukosa fedha kwa PHCF
Kuhusu Uteuzi wake Violet alisema kwamba aliamua kujiuzuru ili kuweza kupumzika. Alisema kwamba uteuzi wake ni Donatian alimpendekeza kwa Tim.
Aidha alisema kwamba matatizo yote yalikwisha na hana tatizo na mtu yoyote katika mtandao.
Maelezo ya Moms in Touch.
Mwanachama aliyefukuzwa alikuwa na Moms in Touch. Pia walimlaumu Tim kwa kuchukua taarifa za mtu mmoja bila kuwaona viongozi wa Moms. Kuhusu risiti feki Moms in Touch hawana utaratibu wa kununua risiti na sababu ya kumfukuza mwanachama si risiti bali ni utovu wa nidhamu.
Mwenyekiti alisema kwambatatizo linaonekana kwa Tim. Hii ni kutokana na kuchukua maelezo ya upande mmoja. Pia lugha inayotumia si nzuri kibinadamu.
Wajumbe wamesema tatizo ni katiba.
Mchakato wa kuibua tatizo la Moms in Touch haukuwa wa haki kwani uliegemea upande mmoja. Tathimini ya maelezo juu ya asasi ni vema yakakubaliwa na pande zote mbili. Suala la Moms in Touch ni kuwajengea uwezo na si kuwanyima fedha. Mtu akifukuzwa ni huwa na hasira hivyo ni rahisi kutoa taarifa za kuharibu asasi aliyofukuzwa.
Kwa sababu hizo mkutano haujaridhia taratibu za kutoa vifaa baada ya fedha. Pia umesema kwamba asasi hizo zinastahili kupewa fedha na kujengewa uwezo.
Tim aulizwe juu ya taarifa za vikundi vilivyopewa na mchakato uliotumika kuwapa vifaa.
Ruzuku ya roborobo
Donatian atakaa na vikundi hivyo kujadiliana ili kuweza kujengea uwezo zaidi juu ya utawala wao. Aiha Donatian atafanya ufuatiliaji wa karibu kwa kushirikiana na viondozi kuhakikisha vikundi hivi vinarekebisha tofauti za kiutawala.
Ruzuku
zilizosimamishwa
CHIYOWONET
Mwenyekiti wa mtandao alimpigia simu mkurugenzi wa CHIYOWONET na mkurugenzi huyo alihoji kwa nini wanazungumzia suala la CHIYOWONET kwani yeye amejitoa katika mtandao. Kikao kiliamua waandikiwe barua na barua watoe maelezo ya kiofisi juu ya hiyo.
IYANA
Imeonekana kwamba kuna tabia ya watu wanaoharibu katika
mashirika
yao
na kuwajibishwa hukimbilia kutoa maelezo ya uongo kwa nia ya kuharibu na kuchafua taswira ya shirika. Mkutano umeona kwamba IYANA wana haki ya kupewa ruzuku.
.
Utaratibu wa kutoa
taarifa.
Kama
kuna taarifa muhimu kwa ajili ya mtandao ni vema Tim akawapatia viongozi mapema ili kuwezesha uchambuzi wa kina wataarifa hizo. Msemaji wa masuala ya mtandao ni mwenyekiti wa Mtandao. Taarifa za kiofisi zifuate mtandao. Mkutano ulijifunza kutoka Argentarian Foundation ambapo msemaji wao mkuu ni Tim Jackson. Na hakuna mtu mwingine anayehusika na mawasiliano. Huu ni utaratibu mzuri ambao asasi zetu zijifunze. Hii inamaanisha kwamba mawasiliano yanayohusu mtandao kiofisi yatafanywa na mwenyekiti.
MFUMO WA MAAMUZI
Kumekuwa na tatizo juu ya mfumo wa maamuzi katika mtandao wa AFCONET. Aidha mkutano uliamua kwamba maamuzi yote yafanywe na mkutano mkuu. Wafadhili wapewe taarifa ya maamuzi.
MRADI WA MAKTABA
NDOGO
Wanachama wamefuridhia maendeleo ya mradi wa maktaba ndogo. Na wameomba fomu zisambazwe.
UKAGUZI WA MAHESABU
Mkutano umeamua kwamba mahesabu yafanywe kwa mashirika yote. Na iwe mwisho wa mwaka ili kuweza kufaya mahesabu ya mwaka mzima.
MENGINEYO
Nauli mtarejeshewa kulingana na umbali. Wajumbe watalipwa kulingana na umbali halisi wa mjumbe.
Kuna asasi mbili zilizopewa cheki za awali. Asasi hizo ni Good Samaritan na YOPAC. Asasi hizo zimetakiwa na mhazini zirejeshe kiasi hicho.
Kufunga kikao.
Kikao kilifungwa na mwenyekiti saa 10:30 jioni. Katiak kufunga kikao mwenyekiti alisema maamuzi yaliyopitishwa ni halali na yataingizwa katika katiba.

Comments